Breaking News

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo Na Mwanasheria Wake Waendelea Kusota Rumande

Aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo Judethadeus Mboya na aliyekuwa mwanasheria wake Andrew Gregory wameendelea kusota mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana katika kesi inayowakabili.

 Wawili hao wanakabiliwa na kesi za kutumia vibaya madaraka na uhujumi uchumi ambapo wanadaiwa kuisababishia Wilaya ya Rombo hasara ya shilingi Milioni 206.

Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Mjini Moshi, Bernaita Maziko na Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro Suzan Kimaro watuhumiwa hao wamekana mashitaka dhidi yao ambapo walitakiwa kupewa dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye kiasi cha shilingi milioni 56 huku wadhimini wengine wawe ni watumishi wa Umma wanaofanya kazi mkoni Kilimanjaro.

Washitakiwa wameshindwa kutimiza mashariti ya dhamana na kurejeshwa mahabusu hadi Februari 8 kesi yao itakaposikilizwa tena.

ليست هناك تعليقات