Breaking News

Alichokisema Kikwete kuhusu kifo cha Ruge Mutahaba hiki hapa




Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ni miongoni mwa walioguzwa na kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Soma zaidi: Wasanii, Watangazaji walivyomzungumzia Ruge Mutahaba

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Kikwete ameandika ujumbe unaomzungumzia Ruge huku akiambatanisha picha waliyopiga pamoja wakiwa na nyuso za furaha.

“Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba,” amesema Kikwete

“Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi katika uongozi wangu na hata baada ya kustaafu.”

“Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Namuombea kwa mola ampe mapumziko mema Peponi. Ameen.” Amesema kiongozi huyo wa awamu ya nne.

No comments