Breaking News

HAWA HAPA WASHINDI WA TUZO ZA ZIFF 2019



Hawa hapa wamejibebea tuzo kwenye tuzo za Sinema Zetu mwaka 2019 zilizofanyika Mlimani City:-


MUIGIZAJI BORA WA KIKE: Tuzo imekwenda kwa Flora Patience Kihombo kupitia movie ya ‘Kesho’.


Filamu Bora yenye Maudhui ya Kitaifa – Filamu iliyoshinda ni SIYABONGA kutoka kwa Salim Ahmed a.k.a Gabo Zigamba.


Sinema Zetu imetoa tuzo kwa filamu ambazo hazijapata tuzo katika vipengele vingine lakini zimefanya vizuri katika mikoa mbalimbali.


MSHINDI – Tuzo ya Mtu Aliyetukuka katika tasnia ya Filamu Tanzania inakwenda kwa Mzee Majuto (ambaye kwa sasa ni marehemu). Tuzo hii imetolewa na majaji.


Filamu Bora upande wa Filamu Fupi – Filamu iliyoshinda ni SUPA MAMA.


Muigizaji Bora wa Kike katika World Cinema – Washindi ni wawili, Leena Alam kutoka Afghanstan na Myra Vishwakarma kutoka India.


Makala Bora – Mshindi ni Adam Juma kupitia makala ya AMKA




Mchekeshaji Bora katika Filamu Ndefu – Mshindi ni Madebe Lidai kupitia filamu ya ‘MAMA MWALI’


Mwandishi Bora wa Muswada – Filamu iliyoshinda ni ‘SUPA MAMA’, mshindi akiwa ni Christina Pande


Mhariri Bora wa Filamu Fupi – Mshindi ni Ibrahim Jabir kupitia filamu ya ‘TAMAA’.


Mpiga Picha Bora Filamu Ndefu – Filamu iliyoshinda ni T-JUNCTION mshindi akiwa ni Lister Millado.


Mpiga Picha Bora katika Filamu Fupi – Mshindi ni Adam Juma katika filamu ya ‘TAMAA’.


Muziki Bora wa Filamu Ndefu – Filamu iliyoshinda ni ‘DEMA’ mshindi akiwa ni Khatwab Khamis.


Muziki Bora World Cinema – Filamu iliyoshinda ni ‘THE SILENT REVOLUTION’.





Muziki Bora wa Filamu Fupi – Filamu iliyoshinda ni SISI NA WAO.

No comments