Kagere apelekea kilio Jangwani
Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ameibuka shujaa baada ya kufunga bao pekee Simba ikichapa Yanga 1-0 kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.
Kagere alifunga bao akimaliza kwa kichwa krosi ya nahodha John Bocco katika dakika 71, na kuwanyamazisha mashabiki wa Yanga.
Kagere amefunga bao lake la tisa katika Ligi Kuu na kuisaidia Simba kufikisha pointi 39, katika nafasi ya tatu wakati Yanga ikibaki kileleni na pointi 58.
Katika mchezo huo Simba ilibadilika kipindi cha pili baada ya Yanga kubadili mbinu yao ya kujilinda na kuanza kushambulia.
Katika dakika 61, Okwi alipiga shuti na kugonga mwamba na kuhamsha makelele uwanjani, hata hivyo wachezaji wa Yanga waliweza kuondoa shambulizi hilo haraka.
Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib hakuonyesha makeke katika mchezo huu hali ambayo iliwafanya mashabiki waanzishe minong'ono uwepo wake uwanjani.
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alifanya mabadiliko kwa kumtoa Ibrahim Ajib na kuingia Mohammed Issa 'Banka' ili kuwenda kuongeza nguvu katika eneo la katikati.
Simba wakishambulia kwa mfululizo lango la Yanga dakika 70, hata hivyo umakini wa Abdallah Shaibu Ninja uliweza kuokoa mashambulizi hayo.
Simba walizidisha mashambulizi na dakika 71, Simba walipata bao baada ya Bocco kupiga krosi iliyomaliziwa kwa kichwa na Meddie Kagere.

No comments