Makamu wa Rais na RC Makonda wawaonya wasanii
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda ameweka wazi kuwa suala la kupambamba na wauzaji wa dawa za kulevya lilimuweka kwenye wakati mgumu na kama sio mkono wa Mungu angeweza kuteketea hata kwa kutupiwa mapepo.
Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 13, 2019 kwenye kongamano kuhusu tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini (DCEA), kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lililofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
''Bila mkono wa Mungu nisingekuwepo, wauzaji dawa za kulevya wakishindwa kukuondoa kwa nguvu zao za fedha wanauwezo wa kukuondoa kwa kutumia waganga wa kienyeji, wakishindwa wanaweza kukutupia mapepo mwisho unaweza kusikia umepata ajali'', amesema Makonda.
Naye makamu wa Rias wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi amewaonya wasanii kutojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya huku akitoa mfano wa matatizo aliyopata mwanamuziki wa Marekani marehemu Whitney Houston.
Awali kabla ya kuanza kutoa hotuba, Makamu wa Rais alianza kwa kutoa pole kwa wasanii kutokana na msiba wa msanii Golden Jacob Mbunda maarufu Godzilla.
“Nimepata taarifa kwamba usiku wa kuamkia leo tumepata msiba wa Msanii mmoja nae ni Ndugu Golden Jacob Mbunda kwa umaarufu ni Godzilla, sasa naomba wote tusimame dakika moja tumpe heshima yake na kila mtu aombe kwa kitabu anachokiamini”, amesema Makamu wa Rais.
No comments