Breaking News

Ruge amponza Dudubaya, Waziri atoa maagizo mazito.


HARRISON Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Jeshi la Polisi, kumchukulia hatua msanii, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya,’ kwa kumdhihaki aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vipindi wa Clouds Media Group, Marehemu Ruge Mutahaba. 

Mwakyembe ametoa agizo hilo leo tarehe 27 Februari 2019, baada ya Dudubaya kusambaza video katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha akimdhihaki marehemu Ruge.
Aidha, Mwakyembe ameitaka BASATA kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua za kisheria Dudubaya kufuatia hatua yake hiyo.
Ruge alifariki dunia jana nchini Afrika Kusini alikokuwa anapatiwa matibabu ya tatizo la figo lililomsumbua kwa zaidi ya miezi minne, ambapo alianza kutibiwa katika Hospitali ya Kairuki iliyoko jijini Dar es Salaam, na baadae akapelekwa India kisha kupelekwa Afrika Kusini ambako umauti ulimfika.

No comments