TANESCO KWA KUSHIRIKIANA NA MKANDARASI ABB TOKA SWITZERLAND KUFUNGA TRANSFOM YENYE MEGAWITI 240
Transfoma hiyo iliingia hapa
nchini mnamo Januari 28, 2019 kwa nia ya kuboresha hali ya upatikanaji
wa umeme wa uhakika na kuleta ufanisi katika usambazaji wa umeme katika
jiji la Dar es Salaam na Pwani.
Akielezea uwezo wa Transfoma
hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi
Joseph Msumali amesema Transfoma hiyo yenye uwezo wa kusukuma takribani
Megawati 240 kutoka kwenye msongo wa kilovoti 220 kuelekea Msongo wa
kilovoti 132 kwa ajili ya usambazaji na matumizi ya nishati ya umeme
katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
No comments