Breaking News

Wafanyakazi tisa wa Wilaya ya Ifakara wamefariki katika ajali Morogoro




Watumishi tisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ifakara wamefariki baada ya gari aina ya Land Cruiser walilokuwa wakisafiria kumshinda dereva na kutumbukia mtoni Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.

Akizungumzia juu ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali.

“Leo (jana) Saa 11 jioni ktk Wilaya Kilombero gari lenye namba za usajili 994 Toyota Land Cruiser mali ya TAWA, gari ilikuwa inaenda Ifakara ilipofika daraja la Mto Kikwawila liliingia kwenye hilo daraja na kutumbukia Mtoni upande wa kushoto”RPC Morogoro Mutafungwa

“Watu tisa wamefariki wa kwanza ni Salome Lucas, Shaban Yusuph, Glory Steven, Ludaya Mwakalebela, Silvester Mwakalebela, Maria Buginja, Sheila Shitambuni, Hassan Kayunga, Msafiri Kerald, hawa ni Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara” RPC Morogoro Mutafungwa

“Dereva wa gari hilo Baraka ambaye ni mzima amekamatwa anahojiwa, chanzo cha ajali ni mwendokasi na uzembe wa Dereva kushindwa kutawala gari akiwa ktk mwendo na kuweza kutumbukia darajani, tukio sio zuri” RPC Morogoro Mutafungwa

No comments