Kocha wa Manchester United atoa kauli hii baada ya kupangiwa na Barcelona UEFA
Leo mchana droo ya robo fainali ya Klabu bingwa barani Ulaya imepangwa, ambapo klabu ya Manchester United ya Uingereza imepangwa na Barcelona ya Hispania kwenye hatua hiyo.
Na baada ya makundi hayo kupangwa leo kocha wa Manchester United Mnorway Ole Gunnar ameongea haya baada ya timu yake kupangiwa na FC Barcelona:- “”Tunataka michezo kama hii dhidi ya klabu kubwa na timu kubwa,” anasema Ole. “Tulikutana mara ya mwisho dhidi yao mwaka 2009 na 2011 na nusu ya mwisho mwaka 2008 wakati Scholesy alifunga goli, ni michezo kama hii mashabiki wetu na klabu yetu inazitamani sana na Tulitarajia hii. “
Aliongeza “Mimi inawezekana nina asilimia 99 ya kuwa kocha wa muda wote hapa, na napendelea zaidi kama tulivyokutana na na PSG. Ikiwa wataweza kupata matokeo mazuri nyumbani, basi tunajua tunaweza kwenda na kuumiza mtu yeyote kama tulivyofanya huko Paris. “
Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.
BOFYA HAPA
No comments