Breaking News

RAIS KENYATTA AFUNGA MPAKA WA KENYA NA TANZANIA



Rais wa Kenya,  Uhuru Kenyatta ametoa amri ya kufungwa mipaka yote ya Kenya inayopakana na Tanzania kwa siku 30 kuanzia leo. Mipaka hiyo ni pamoja na Namanga, Isebania, Horohoro, Holili na Tarakea-Rombo. Utekelezaji wa amri hii ya Rais unaanza rasmi leo saa sita kamili za usiku.

Aidha Kenyatta pia ametoa amri ya kufungwa kwa mpaka wa Kenya na Somalia.

Rais pia ametangaza kuwa zuio la kutotoka ndani limeongezwa kwa siku zingine 21 zaidi.

Kenyatta amebainisha kuwa mipaka yake na nchi zingine ikiwemo Uganda, Ethiopia na Sudan Kusini itaendelea kuwa wazi na shughuli zitaendelea kama kawaida kulingana na makubaliano waliyoafikiana katika kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Heads of State) mkutano ambao Tanzania na Burundi hawakushiriki ambapo safari za Rwanda-Kenya zitafanyika kupitia Uganda. 

Amri hii ya Rais Kenyatta inajiri siku chache tu baada ya amri sawia na hio ya kufunga mpaka wa Tanzania na Zambia (Tunduma-Nakonde border) kutolewa na Rais Edgar Lungu wa Zambia.

Itakumbukwa kuwa siku za hivi karibuni Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitoa taarifa kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa amefanya mazungumzo na Marais Uhuru Kenyatta na Paul Kagame kuhusu namna ya kupambana na Corona Virus katika mipaka na wamefikia makubaliano mazuri hata hivyo alijadiliana na Rais John Magufuli wa Tanzania jambo tofauti kidogo.

No comments