Breaking News

Mazishi Ya Baba Kiba Yakamilika Mwenyewe Afunguka Haya..

Safari ya Baba mzazi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi "Ali Kiba" mzee "Saleh Kiba imefikia tamati jana baada ya mazishi kukamilika.

Mzee Kiba alifariki jana na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam huku mazishi hayo yakihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu...


Miongoni mwa eatu waliohudhuria ni pamoja na Dkt. Kigwangala, Mr Blue, Dully Syeks, Mwana FA na wengine wengi.

Hata hivyo baada yote hayo kutokea msanii huyo nguli wa muziki ameandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa instagram akiwashukuru wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine katika safari ya kuhifadhi mzazi wake.

"Nawashukuru wote walioshiriki katika mazishi ya mzee wangu Na wale ambao hawakujaaliwa pia mimi Na familia yangu tumefarijika sana namuomba MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali Pema peponi Na atupe subira kwenye kipindi hiki kigumu  AMIN"

No comments