NKANA MABINGWA MARA MBILI MFULULIZO NGAO YA JAMII:
Timu ya Nkana fc imefanikiwa kutwaa kombe la ngao ya jamii Inayofahamika kama [ Samuel’ Zoom’ Ndhlovu Charity ] baada ya kuifunga Zesco utd kwa mikwaju ya penati 5-4 kufuatia mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo huo unaoashiria ufunguzi wa ligi ya Zambia inayofahamika kama Super league.
.
. -Ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho kwa michezo kadhaa kuchezwa ambapo pia ikumbukwe ligi hiyo imegawanywa katika makundi mawili , kundi A na kundi B huku Zesco ikiwa impangwa kundi A na Nkana red devils ikiwa imepangwa kundi B.
.
.
Bao la Zesco utd limefungwa na
Maybin Kalengo dakika ya 2 huku bao la nkana likifungwa na Ronald Kampamba dakika ya 46

No comments