RC MWANRI ATOA ONYO KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA WANAOCHUKUA FEDHA KWA MAMA MJAMZITO

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameahidi kuwashughulikia wataalam wa afya wanaowatoza fedha wajawazito wakati kutaka kujifungua.
Pamoja na mambo mengine amesema kwa sasa wanaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya pamoja na kupunguza vifo vya mama na mtoto mkoani humo.
Akizungumza katika kampeni za Bima ya Afya ya Jamii(CHF) iliyoboreshwa pamoja na Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe salama ,Mwanri ametumia kampeni hizo kuwanyooshea vidole baadhi ya watoa huduma za afya ambao wanawatoza fedha wanawake wajazito wanakwenda kujifungua katika vituo vya afya na zahanati.
Mwanri amesema hatosita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi wa afya atakayebainika kumtoza fedha mama mjamzito.
Katika hatua nyingine Mwanri ametoa onyo kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani humo ambao wamezembea kuwasajili wazee na kufungua madirisha maalum ya kuwahudumia katika hospitali na zahanati zilizopo kwenye maeneo yao.
Kuhusu uzinduzi wa kampeni hizo imekwenda pamoja na Serikali ya Mkoa wa Tabora kupokea magari madogo nanne ya kubeba wagonjwa kutoka Shirika Care International kupitia mradi wa Tamani yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 184.
No comments