Breaking News

Barua Ya Wazi Ya Mwl Kashasha Kwa Shaffih Dauda

Mchambuzi wa soka nchini, Mwl Alex Kashasha amemtolea uvivu mchambuzi mwenzie, Shaffih Dauda juu ya misimamo yake na namna ambavyo amekuwa akionyesha waziwazi kuwa upande fulani wa timu.

Kwa mujibu wa barua ya wazi aliyoiandika kwenda kwa Shaffih Dauda, Mwl Kashasha amesema kuwa anasikitishwa na kile kinavhoendelea kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Hii hapa Barua yenyewe.


#AnOpenLetterTo @shaffihdaudatz nimesikitishwa sana kwa kinachoendelea mtandaoni especially kwa mtu wa taaluma kama yako unaidhalilisha fani hii ya uandishi na uchambuzi wa mpira umekua provoked na umereact now people know who you are which sio kitu kizuri kwa mtu wa aina yako mwandishi especially mchambuzi wa habari za michezo sio tu Tanzania Bali Duniani kote  hapaswi kutake sides kwasababu ya Kua na effects nyingi negative than positive ones kwamfano mashabiki wa @simbasctanzania hata uje useme nn itakua ni ngumu kwao kurudisha imani kwako And most of the people ambao labda kwa namna moja ama nyingine sio wapenzi wa timu hizi mbili bado watakuona sio mtu sahihi kwao kupata habari za uchambuzi wa michezo kwasababu tu watahisi tayari upo biased unaweza ukaona upo sawa kwamba unataka kumprove @hajismanara wrong kwamba @simbasctanzania ni underdog but unaiua career yako ambayo umetumia miaka mingi kuitumikia na kupata mafanikio in this field working as a football analyst kuna one simple rule #dontEverLetFansDiscoverWhichSideYouAre just let them have their doubts but they shouldn't prove their doubts from you kitu ambacho wewe umefeli kwamfano najua wewe ni shabiki wa @manchesterunited sio kwamba nimeambiwa hapana ni kutokana tu na weledi wangu na namna unavyoreport habari zao
Lakini haijawai kuwakera mashabiki wa timu nyingine za premierleague unajua ni kwanini?
Kwasababu ulifanya ionekane kama part ya taaluma yako
Kitu ambacho umeshindwa kwa suala hili la @simbasctanzania ni aibu kwa mwandishi mkubwa na mwenye uzoefu kama wewe kuwa na attitude ulioionyesha
Mambo hayo ni ya mashabiki na sio ya kufanywa na mtu kama wewe
Naskia kuna kipindi flani ulikua unataka kugombea nafasi ya uongozi @tanfootball imagine umepata nafasi ya juu labda uraisi alafu inatokea mzozano unaoihusu @simbasctanzania kwa namna moja ama nyingine wakihisi kuonewa nani atapewa lawama hizo
Kutokana na hichi kinachoendelea?

No comments