Breaking News

Kikosi Cha Al Ahly Kitakacho Wavaa Simba Leo

Related image

Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly, Martin Lasarte ametaja kikosi cha Wachezaji 18 tu kitakachoshuka Dimbani kucheza Mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mabingwa wa Tanzania, klabu ya Simba SC.. Mechi hii Ni ya tatu kwa kila timu huku Ahly wanaingia Kama Vinara wa Kundi D Katika Michuano hii ya CAF Champions League wakiwa na Pointi zao Nne.
.
- Baada ya Ushindi nyumbani dhidi ya AS Vita Club, Sare Ugenini dhidi ya JS Saoura, Katika Mechi mbili zilizopita na Mechi ya tatu hii leo wanawaalika Mabingwa wa Tanzania Klabu ya Simba SC ambao wapo nafasi ya tatu na pointi zao tatu wakishinda Mechi moja nyumbani dhidi ya JS Saoura na kupoteza Ugenini Nchini DR Congo dhidi ya AS Vita Club.
.
- Kwa Al  Ahly anarejea Beki wao, Rami Rabiaa kufuatia kuwa nje kwa majeruhi, pia baada ya kuugua Nahodha wa Miamba hao Hossam Ashour yupo fiti kuikabili Simba, kwa upande mwingine Red Devils hawatokuwa na Wachezaji wao wengine Yasser Ibrahim, Ramadan Sobhi na Islam Mohareb kwa majeruhi tofauti tofauti... Kwa upande wa Simba SC hakuna Majeruhi aliyeripotiwa kukosa Mechi hii Katika Orodha kamili ya Wachezaji 20 waliosafiri kuelekea Misri.
.
- KIKOSI KAMILI CHA AL AHLY KINACHOIVAA SIMBA SC.
MAKIPA: Sherif Ekramy, Mohamed El-Shennawy.
.
MABEKI: Mohamed Hany, Saad Samir, Ayman Ashraf, Rami Rabiaa, Ali Maaloul, Mahmoud Wahid.
.
VIUNGO: Amr El-Sulaya, Hesham Mohamed, Hossam Ashour, Karim Nedved, Mohamed Sherif, Ahmed Hamoudi, Nasser Maher, Hussein El-Shahat.
.
WASHAMBULIAJI: Junior Ajayi, Salah Mohsen.

No comments