Breaking News

BREAKING: Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia



Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo, taarifa ya Clouds Radio imeeleza.

Kifo cha mtangazaji huyo kinakuja siku chache baada kufariki Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media,Ruge Mutahaba.



Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa Mkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #RugeMutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Mtangazaji wetu #EphraimKibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7 2019)

Tunamtukuza Mungu kwa Maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu.  Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe. Tunamtukuza Mungu kwa Maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.

No comments