Wananchi wa Ilongero wamshukuru Rais Magufuli
Wananchi wa Ilongero Wilayani Singida wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa maamuzi yake ya kuwajengea Hospitali ya Wilaya.
Pongezi hizo zimetolewa na wananchi hao wakati wa ziara yake leo ya kikazi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati akikagua miradi ya barabara, afya na elimu Mkoani Singida.
Mhe Jafo ameutaka uongozi wa Wilaya na Mkoa wa Singida kuongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilaya, Mkoani Singida.
Mhe Jafo amepongeza kazi nzuri iliyofanywa ya ujenzi wa mabweni mawili na vyumba vya madarasa vinne, vyoo na ofisi mbili za walimu katika shule ya Sekondari ya Ilongero.
Ameutaka uongozi wa Wilaya kuharakisha ujenzi wa bwalo na maktaba baada ya kupokea fedha nyingine shilingi milioni 150 kwa ajili ya miundombinu hiyo.
Mhe. Jafo amewapongeza sana waalimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa matokeo ya kutia moyo ya kidato cha sita ya mwaka jana baada ya wanafunzi wote kufaulu kwa madaraja mbalimbali bila hata mmoja aliyepata daraja sifuri.
Jafo amehitimisha ziara yake kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mkoani Singida

No comments