Breaking News

GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEO LENYE HEKARI HIZI



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kwamba wana mpango wa kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo katika eneo la ukubwa wa hekari 15. 

Gambo ameyasema hayo leo asubuhi wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) mjini Arusha. 

“Serikali ya Mkoa wa Arusha tumetenga hekari 15 kwa ajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo na TFF ndiyo watakaousimamia bila kupata usumbufu,”alisema Gambo. 
Akifungua mkutano huo, Gambo aliwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kuheshimu mamlaka akisema kuwa hata kama kuna mtu haridhiki na utawala wa sasa wa TFF, hana budi kuiheshimu kwani mamlaka hiyo imewekwa kihalali na inatambuliwa na Serikali. 

“Uchaguzi mlishafanya na tunajua safu ya uongozi ilishakamilika lakini bado kuna watu wanataka kuirudisha TFF ilikotoka. Ombi langu kwenu ni msikubali”, alisema Gambo.

No comments