Breaking News

Magari ya waya kupandisha watalii Mlima Kilimanjaro

Picha

KAMPUNI mbili za China zimeonesha nia ya kuanzisha magari ya waya yatakayokuwa yakiendeshwa kwa umeme kwa ajili ya kupandisha watalii katika Mlima Kilimanjaro. Hayo yamesemwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA), Beatrice Looiboki wakati akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (pichani) ambaye yupo ziarani katika hifadhi hiyo.

Alisema kwamba mazungumzo na kampuni hizo yanaendelea. Wakati mhifadhi anatoa taarifa hiyo,Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inatarajia kuanza mkakati maalumu wa kuongeza idadi ya watalii wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelelea ukiwemo wa kuanzisha magari yatakayokuwa yakitembea kwenye waya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Alisema kama nchi imekuwa ikikosa pesa nyingi zinazotokana na watalii wa kundi hilo ambao ndio wengi wanaokuja nchini kwa ajili ya kutalii mara baada ya kustaafu. Aliongeza kuwa, magari hayo yatasaidia kukuza utalii hata kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kufika katika kilele cha Mlima huo.

Aidha, Kanyasu amesema serikali inategemea kujenga viwanja vya ndege vikubwa kwa baadhi ya hifadhi ikiwemo Selous pamoja na Ruaha, ikilenga kundi la watalii wenye bima za maisha ambazo zinawaruhusu kusafiri kwenye ndege kubwa na zenye marubani wawili, hali itakayopelekea kutua moja kwa moja katika hifadhi hizo tofauti na ilivyo sasa.

Kanyasu akizungumza na Menejimenti ya Uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika ziara yake ya kikazi wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro pia alisema Serikali imeanza kupitia malalamiko ya baadhi ya wadau wa utalii wa ndani ya nje ya nchi kuwa utalii wa Tanzania ni wa ghali sana ukilinganisha na nchi nyingine. Kama serikali, tumeamua kuanza kulifanyia kazi suala hili kuwa "Tanzania is an expensive destination" lengo letu likiwa ni kuongeza idadi ya watalii pamoja na mapato ambayo ni lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano
   







No comments