Breaking News

MAJERUHI 10 WA AJALI YA BASI FRESTER WAMEENDELEA KULAZWA HOSPITALI TEULE BIHARAMULO.

Image may contain: one or more people, people sitting and indoor


Majeruhi wa basi ya Frester wameendelea kulazwa hospital teule Biharamulo baada ya 32 kuruhusiwa na wengine kuomba kutibiwa karibu na makazi ya maeneo wanayotoka . watatu wamepata rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa Bugando.
Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Biharamulo, Dkt Edgar Zabron amewataja waliopelekwa Bugando kuwa ni Benitha Burchard (22) na Mathilida Yohana (61) ambapo walivunjika mikono upande wa kulia kila mmoja na Gezila Raulian aliumia kiuno.
Wawili waliobaki wanahitaji wataalam wa mifupa baada ya kuumia mikono.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Kagera Isack Msengi amefafanua chanzo cha ajali ni mwendo kasi , Dereva Benjamin Magida (43) alishindwa kukata kona iliyopo kijiji cha Kasuno kata ya katahoka majira ya saa 3: 10 hatimae kupinduka. Gari lilikuwa na abiria 53.
 Image may contain: one or more people and outdoor

No comments