Mourinho Ahukumiwa Kifungo
Kocha wa zamani wa klabu ya kandanda ya Real Madrid na Manchester United Jose Mourinho amepewa hukumu ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja baada ya kukubali kuwa ana hatia kwa udanganyifu wa kodi nchini Uhispania leo. Mourinho hatatumikia kifungo jela baada ya kukiri kufanya udanganyifu kwa maafisa wa Uhispania mwaka 2011 na mwaka 2012. Kama sehemu ya mpango huo pia atawajibika kulipa faini ya euro milioni 2.

No comments