Breaking News

Nahodha Simba atamba kulipa kisasi kwa Al Ahly



MTANANGE wa michuano ya Klabu Bingwa kati ya timu ya Simba na Al Ahly ya Nchini Misri unatarajiwa kuchezwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Kuelekea mechi hiyo, Nahodha wa timu ya Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kuwa anaamini mchezo huo utakuwa ni mgumu kwao ila watahakikisha wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani. Tshabalala amesema, katika mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli nyingi sana ila alama zinazopatikana ni tatu kwahiyo wao kama wachezaji wamejizatiti kuweza kupata alama hizo wakiwa nyumbani.


“Tunaamini mchezo wetu wa kesho tunashinda na kikubwa ushindi wowote tutakaoupata alama ni zile zile tatu, ingawa wao walitufunga kwa goli nyingi ila sisi tutatumia uwanja wetu wa nyumbani kupata matokeo,”amesema. Amesema, kikubwa ni wachezaji kujituna uwanjani katika dakika zote 90 na pia mashabiki kujitokeza kwao kwa wingi uwanjani ni moja ya hamasa kubwa sana kwao.


Kwa upande wa Kocha Mkuu wa klabu ya Al Ahly kutoka Uarabuni amesema haiofii klabu ya Simba kwani waliweza kupata matokeo wakiwa nyumbani kwa ushindi mnono wa goli tano na wanaamini wanaweza kushinda tena hata wakiwa ugenini.


Simba atashuka tena dimbani na Waarabu mapema kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo katika kundi D Al Ahly amekuwa kinara kwa kuwa na alama 7 akifuatiwa na Alh Alhy mwenye alama 4, Simba akishika nafasi ya tatu kwa alama 3 na JS Saoura akiwa na alama 2. Ikumbukwe katika mchezo wao kwa kwanza uliopigwa Februari 02 dhidi ya Al Alhly Simba alikubali kupigo cha goli 5-0 akiwa ugenini nchini Misri

No comments