NAIBU WAZIRI NDITIYE AKABIDHI KOMPYUTA SHULE ZA SEKONDARI MPANDA
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati)
akikabidhi kompyuta kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi (wa
pili kulia) kwa ajili ya shule za sekondari mjini humo. Wakishuhudia, wa
kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa
Wote, Mhandisi Albert Richard na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,
Abdallah Malela (wa pili kushoto)
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua
jambo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
na waalimu wa sekondari (hawapo pichani) kuhusu ukuaji na maendeleo wa
sekta ya Mawasiliano nchini. Kulia kwake ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe.
Sebastian Kapufi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,
Abdallah Malela.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Albert Richard
akitoa maelezo ya kompyuta walizotoa kwa shule za sekondari za Mpanda.
Walioketi wakimsikiliza, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni Mbunge wa
Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi.
Afisa
Elimu wa Shule za Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu
akisoma risala ya shukrani kwa Serikali kwa niaba ya waalimu na
wanafunzi wa shule kwa kuzipatia shule hizo kompyuta 25. Walioketi
wakimsikiliza wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni Mbunge wa Mpanda
Mjini, Sebastian Kapufi.
Waalimu
wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi na
Manispaa ya Mpanda wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati
akiwahutubia kabla ya kukabidhi kompyuta kwa ajili ya shule za sekondari
za Mpanda.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
akisisitiza jambo kwa Afisa Usalama Msaidizi wa Uwanja wa Ndege wa
Katavi, Fredrick Valentine(wa kwanza kulia) wakati akikagua miundombinu
na hali ya uwanja huo akiwa ziarani mkoani humo. Mbunge wa Mpanda Mjini,
Sebastian Kapufi (wa tatu kulia) akifuatilia kwa makini mazungumzo
hayo.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
(aliyesimama mbele amefunga mikono) akiwa kwenye picha ya pamoja na
waalimu wa shule za sekondari, viongozi na watendaji wa mkoa wa Katavi
na Manispaa ya Mpanda. Wan ne kulia ni Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian
Kapufi na wa tano kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Abdallah
Malela
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amekabidhi
kompyuta 25 kwa shule za sekondari Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la
kukuza kiwango cha ufaulu na kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) shuleni kwa kuwawezesha waalimu kutumia
kufundishia na wanafunzi kujifunzia
Nditiye
amewataka waalimu na wanafunzi wa shule hizo kuhakikisha kuwa kompyuta
zilizotolewa zinatumika kwa nia njema kutoa elimu kwa watoto wetu kwa
kuwa sasa dunia ni kijiji.
Amefafanua
kuwa lengo ni tupate wanafunzi mahiri kwa kompyuta hizo kutumika na
wanafunzi wengine kwenye shule mbali mbali kwa kuziunganisha kompyuta
hizo kwenye mtandao ili mwalimu mmoja aweze kufundisha wanafunzi wengi
wengine wa shule nyingine
“Kumbukeni
hapo zamani wanafunzi wa mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ilikuwa
inatoa wanafunzi wenye ufaulu mzuri, hivyo tuwarithishe wanafunzi wetu,”
amesisitiza Nditiye
Kompyuta
hizo zimetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao una dhamana ya kuhakikisha
wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wana
wasiliana kwa kuzipatia kampuni za simu za mkononi ruzuku ya kujenga
minara ili kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbali mbali nchini
Nditiye
amekabidhi kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 46 kwa Mbunge
wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kwa niaba ya waalimu na wanafunzi
wa shule za sekondari zilizopo mjini humo kwa kuwa aliiomba Serikali
kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu ili shule hizo ziweze kupatiwa
kompyuta hizo.
“Nimeanza
kumsumbua Nditiye zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuomba kompyuta, unaweza
kuona kompyuta ni chombo chepesi ila sio hivyo kwa kuwa ni chombo
muhimu na kitatunza siri,” amesema Kapufi
Pia,
ameongeza kuwa tunalotekeleza hapa ni upendo na na litaenda kufuta
ujinga wa watoto wetu kwenye shule za sekondari kwa kutumia kompyuta
hizi. Vile vile ameishukuru Serikali kwa ahadi ya mafunzo ya kompyuta
ambayo yatatolewa kwa waalimu wa shule ili kuwawezesha namna ya kutumia
na kufanyia matengenezo madogo madogo kompyuta hizo ambapo ameahidi kuwa
atakwenda yeye mwenyewe binafsi kukabidhi kompyuta hizo kwa kila shule
Naye
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema
kuwa UCSAF imekuwa ikitoa kompyuta hizo kwenye shule mbali mbali nchini
kupitia mradi wa kuunganisha shule ujulikanao kama “School
Connectivity”. Richard amesema kuwa ni imani yao kuwa kompyuta hizo
zitatumika kwa malengo yaliyopangwa kwa nia ya kuwasaidia wanafunzi
kusoma na waalimu kufundishia. Ameongeza kuwa UCSAF itatoa mafunzo kwa
waalimu wa shule za sekondari za Mpanda ya namna ya kutumia kompyuta
hizo kufundushia pamoja na waalimu wao wenyewe kuweza kuzifanyia
matengenezo madogo madogo kompyuta hizo pale zinapoharibika.
Akizungumza
kwa niaba ya waalimu wa shule za sekondari za Mpanda, Afisa Elimu
Sekondari wa Manispaa ya Mpanda, Enelia Lutungulu amesema kuwa shule za
msingi na sekondari zina uhitaji mkubwa sana wa kompyuta kutokana na
maendeleo ya sayansi na teknolojia na TEHAMA ambapo kazi nyingi
zinahitaji mawasiliano kwa kutumia kompyuta
“Shule
hizi zina uhitaji mkubwa wa kompyuta kwa kuwa baadhi ya shule kompyuta
zinazotumika ni za waalimu binafsi na hivyo kuleta ugumu wa utendaji wa
kazi wa kila siku ukizingatia upokeaji na utoaji wa taarifa ni wa kila
mara,” amefafanua Lutungulu.
Ameongeza
kuwa kompyuta hizo zitakuwa kichocheo cha kuongeza na kurahisisha
ufanisi wa kazi katika shughuli mbali mbali zikiwemo za uchapishaji wa
mitihani ndani ya shule, ukusanyaji na uhifadhi wa data za kielimu
katika shule, utoaji rahisi na wa haraka wa taarifa kwa kutumia TEHAMA,
kupokea miongozo na maagizo mbali mbali ya kikazi kwa kutumia
mawasiliano ya barua pepe, kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na
teknolojia ikiwemo TEHAMA na mawasiliano katika kazi za kila siku.
Makabidhiano ya kompyuta hizo yamehudhuriwa na wakuu wa shule za
sekondari, viongozi na wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na
Wilaya ya Mpanda na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya hiyo
Akiwasilisha
taarifa ya mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Abdallah Malela amemuomba
Nditiye kuipatia mkoa huo ofisi ya TTCL ya ngazi ya mkoa tofauti na hali
ilivyo sasa ambapo ipo ofisi ya TTCL ya ngazi ya wilaya. Pia, ameongeza
kuwa mkoa upatiwe usafiri wa ndege kwa kuwa ina kiwanja kizuri na kuna
wateja wa kutosha
Nditiye
amepokea changamoto hizo na kuielekeza Bodi ya TTCL na menejimenti yake
kufungua ofisi ya Shirika hilo lenye hadhi ya mkoa ndani ya kipindi cha
mwezi mmoja. Pia, ameuhakikishia uongozi wa mkoa na wananchi wa Katavi
kuwa Serikali inaleta gari la zimamoto kwenye uwanja huo na huduma za
usafirishaji utaanza kutolewa kwa wananchi na wadau wa mkoa huo. Pia,
Nditiye alitembelea na kukagua kiwanja hicho cha ndege na kuona hali ya
kiwanja na miundombinu yake.
No comments