Breaking News

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile amelaani mauaji na matendo ya kikatili yote yanayofanywa dhidi ya Watoto

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile amelaani mauaji na matendo ya kikatili yote yanayofanywa dhidi ya Watoto, huku akivishukuru vyombo vya Dola kwa hatua za haraka wanazoendelea kuchukua katika kudhibiti matukio hayo.

Ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya Makazi ya Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  akizungumza na baadhi ya watoto waishio katika Mazingira magumu waliopo Makazi ya Watoto ya Kurasini jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara leo katika makazi hayo.




Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  akifungua bomba la maji wakati akikagua mazingira ya Makazi ya Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara leo katika Makazi hayo.








Naibu Waziri wa Afya, (kushoto) akihakikisha kuwa watoto wanapatiwa chakula bora kwa kukuroga chakula wakati alipofanya ziara yake leo katika Makazi ya Watoto yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam kulia ni Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Beatrice Mgumiro




Naibu Waziri wa Afya,(kulia) akikagua mazingira ya Makazi ya Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu yaliyopo Kurasini jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara leo katika makazi hayo kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Beatrice Mgumiro





Naibu Waziri wa Afya, (kulia) akijadiliana jambo na Afisa Mfawidhi wa Makazi ya watoto waishio katika mazingira magumu Kurasini Beatrice Mgumiro wakati alipokuwa akikagua mazingira wanamolala watoto wakati alipofanya ziara yake leo katika Makazi hayo jijini Dar


No comments