Ratiba ya michuano ya CECAFA yatangazwa
Baraza la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), limetoa ratiba ya michuano yake mbalimbali itakayofanyika mwaka huu baada ya kikao kilichofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
Katika kikao hicho kilichofanyika Februari 10-11, kimetoa maamuzi mbalimbali ikiwamo ratiba ya kufanyika kwa mashindano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kagame Cup’ imepangwa kufanyika Julai nchini Rwanda.
Aidha, michuano ya Chalenji kwa timu za taifa yenyewe itafanyika Desemba nchini Uganda huku kuanzia Juni mpaka Desemba itafanyika michuano ya vijana U-17 itakayofanyikia Eritrea, U 17 kwa wanawake ikifanyika Kenya, wakati U-20 kwa wanawake itafanyika Uganda huku michuano ya timu kubwa za wanawake ikifanyika Tanzania.
Hata hivyo, wanachama wa Cecafa wametakiwa kuchangia kufanikisha kufanyika kwa michuano ambayo haina wadhamini ukiondoa ile Klabu Bingwa inayodhamini [Kagame Cup] inayodhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Azam Media.
No comments