Breaking News

Samsung: Simu mpya ya Galaxy Fold ni kifaa cha 'kifahari'


Kampuni ya simu ya Samsung imezindua smartphone mpya aina ya Galaxy Fold na 5G Galaxy S10.

Galaxy Fold inatarajiwa kuingia sokoni katika muda wa miezi miwili mapema kuliko vile ilivyotarajiwa.

Galaxy S10 5G inatajwa kuwa moja ya simu kubwa ambayo imewahi kutengenezwa na kampuni ya Samsung na inakuja na progamu za kusifika.

Kampuni ya Samsung inasema kuwa Galaxy Fold inauwezo wa kufunguka kwa hadi inchi 7.3 (18.5cm) na kuendesha apps tatu kwa wakati mmoja.

Galaxy Fold inauwezo wa kufunguka kwa hadi inchi 7.3 (18.5cm) na kuendesha apps tatu kwa wakati mmoja.

Samsung imeongeza kuwa programu za Whatsapp, Facebook, YouTube na Microsoft Office zitasawazishwa ili kufanya kazi kwa ubora zaidi katika simu hii mpya.

Imesema kuwa wameunda mfumo mpya ambao unafanya kazi ya kuhimili maelfu ya kurasa zitakazo kunjwa bila kuathiri utenda kazi wa simu yenyewe.



Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia nchini Korea Kusini imesema simu hiyo ina kamera sita- tatu za nyuma three, mbili za upande na moja ya mbele- kuhakikisha inaweza kupiga picha bila kujali imeshikiliwa vipi.

Mfumo wa 4G wa Galaxy Fold unatarajiwa kuwa madukani kuanzia Aprili 26 na itauzwa kwa bei ya dola 1,980 (£1,515).

Samsung imeielezea simu hii mpya kama kifaa cha ''kifahari''

"Fold itawapatia watumiaji wake thamani ya technolojia mpya hasa wale wanaopenda simu zilizo na skrini kubwa bila kuharibu ubora wake," alisema Carolina Milanesi mmoja wa washauri wa masuala ya ubunifu wa teknolojia.
 Simu hii inapatikana kwa rangi nne

Simu hii imepokelewaje?

Baadhi ya wadadisi wa masuala ya teknolojia wanatilia shaka uwezo wa simu hiyo mpya.

"Kinadharia simu hii inavutia sana: zina uwezo wa kupunguza skrini kubwa kuwa ndogon," alisema Neil Mawston afisa kutoka kampuni ya utafiti ya Strategy Analytics.

"Lakini ukweli wa mambo ni kuwa wateja hawana uhakika wa jinsi itakavyofanya kazi, na programu zake bado hazijaimarishwa vilivyo'


Kuna hofu simu hiyo huenda ikawa nzito, betri yake ikawa moto zaidi na bei yake ikawa ghali zaidi.

Kuna ubunifu wowote katika uundaji? utendakazi wake? Binafsi, naona Samsung walikuwa na uwezo wa kuongeza juhudi zaidi- lakini ni simu nzuri kwa wateja wanaotaka mabadiliko.

Bila shaka watu wnaisubiri kwa hamu kubwa ya kuiona hata kama hawatakuwa na uwezo wa kuinunua .


Uzinduzi wa simu hii unakuja siku kadhaa kabla ya kongamano la simu ya mkononi duniani litakaloandaliwa mjini Barcelona.

Washindani wa Samsung wanatarajiwa kuzindua simu zao mpya za aina smartphone.

Mauzo ya smartphone yalipungua mwaka 2018, lakini Samsung iliathirika zaidi baada ya Huawei na kampuni zingine za uundaji simu za China kuwavutia wateja zaidi.

No comments