Breaking News

Simba SC Vs Yanga SC kazi ipo leo Taifa



Hatimaye ile siku iliyokuwa ikingojewa na wapenda soka nchini imewadia, Ni pale miamba ya soka nchini Simba SC na Yanga SC watakaposhuka dimbani kuzisaka pointi.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) unatarajiwa kuchezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam majira ya jioni.

Utakumbuka kwamba mchezo wa kwanza msimu huu Simba SC walikuwa wenyeji Uwanja wa Taifa na dakika 90 zilikamilika kwa suluhu ya kutofungana.

Hadi sasa Yanga SC wanaongoza ligi wakiwa na pointi 58 kibindoni baada ya kucheza michezo 23 huku Simba SC wakiwa nafasi ya tano baada ya kucheza michezo 15 wakiwa nafasi pointi 36 pekee

No comments