Breaking News

TANZIA: Mwanafunzi wa wa kidato cha tatu ajitia kitanzi kwa kutumia tai



 Shughuli za masomo katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Butere Kaunti ya Kakamega zilivurugika kwa muda Ijumaa, Februari 15 baada ya mwanafunzi kupatikana ameaga dunia. 

Mwili wa mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu ulipatikana ukining’inia kitandani katika moja ya mabweni ya shule hiyo. 


Mwili wa mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu ulipatikana ukining’inia kitandani katika moja ya mabweni ya shule hiyo.


Wanafunzi wenzake ndio walioupata mwili huo walipokuwa wakirejea katika bweni hilo baada ya kufanya mtihani asubuhi. 

Kwa mujibu wa Citizen Digital, timu ya maafisa wa polisi kutoka kaunti walifika katika shule hiyo na kufanya kikao na walimu huku waandishi wa habari wakizuiliwa kuingia. 


Usimamizi wa shule hiyo uliwaambia wanahabari wangewapa ripoti kamili kuhusu tukio hilo mara baada ya ukaguzi wa vyombo husika kukamilika. 

Kulingana na barua aliyoiacha marehemu, alihofia kufukuzwa shuleni kwa sababu ya kosa dogo alilolifanya na hivyo kujitoa uhai.


Visa vya kujiua vimekuwa vikiendelea kuwa vingi kote nchini hasa miongoni mwa vijana huku masuala yakianza kuibuka kuhusu tatizo hilo.

 Mnamo Novemba 2018, mtahiniwa katika Shule ya Sekondari ya Alidina Visram jijini Mombasa alijiua baada ya kupatikana na bangi shuleni humo. 


Ripoti ya polisi inasema kwamba, karibia watu 80 walijiua mwezi Oktoba, 2018 pekee.

No comments