Waziri Mkuu Akaribisha Wawekezaji Nchini......Awahakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi za India,
Misri na Falme za Kiarabu waje wawekeze nchini na Serikali itawapa
ushirikiano wa kutosha.
Ameyasema
hayo jana (Ijumaa, Februari 16, 2019) wakati alipokutana kwa nyakati
tofauti na mabalozi wa India, Misri na Falme za Kiarabu wanaowakilisha
nchi zao hapa Tanzania.
Mabalozi
aliokutana nao ni Balozi Sandeep Arya (India), Balozi Mohamed Abulwafa
(Misri) na Balozi Mohammad Albahri (Kaimu Balozi wa Falme za Kiarabu
nchini Tanzania).Akizungumza na Mabalozi hao Ofisini kwa Waziri Mkuu,
Magogoni, Dar es salam, Waziri Mkuu amesema Tanzania ipo tayari
kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi hizo.
Amesema
Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda nchini ili kukuza
uchumi na kufikia wa kati ifikapo 2025, hivyo amewakaribisha
wafanyabiashara waje wawekeze.Amesema Ofisi yake kupitia Waziri mwenye
dhamana ya Uwekezaji, Bibi Angela Kairuki iko tayari kuwasikiliza na
kuwasaidia wawekezaji wote wanaokusudia kuwekeza nchini.
“Tanzania
iko tayari wakati wote kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wawekezaji
watakaojitokeza kuwekeza nchini wanafanikiwa ili mataifa yote yaweze
kufaidika.”Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya
utalii ikiwa ni pamoja na uwepo wa mlima Kilimanjaro, mbunga zenye
wanyama wa aina mbalimbali na fukwe nzuri.
Hivyo,
ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watalii kutoka mataifa mablimbali
yakiwemo yaIndia, Misri na Falme za Kiarabu waje nchini na kutembelea
vivutio vya utalii vilivyopo.
Kwa
upande wao,Mabalozi hao wameishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri
uliopo baina ya Tanzania na nchi zao, hivyo wamemuhakikishia Waziri Mkuu
kwamba watauendeleza.
Wamesema wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa.
Pia Mabalozi hao wameahidi kushirikiana na Serikali Tanzania kuhakikisha inaboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini.
Wamesema wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa Serikali wa kukuza uchumi kutoka wa chini kwenda wa kati kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa.
Pia Mabalozi hao wameahidi kushirikiana na Serikali Tanzania kuhakikisha inaboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments