Wachimbaji wadogo kufikishiwa umeme kwenye mashimo yao
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema kuwa wachimbaji wadogo mkoani Geita wanatarajiwa kufikishiwa Umeme katika mashimo yao ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa ufanisi mkubwa.
Waziri ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita na kusema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika maendeleo ya nchi na kwa sasa umeme utafikishwa katika mashimo ya wachimbaji ili kurahisisha shughuli zao za uchimbaji.
“Ndugu zangu wachimbaji tumeshaanza kuwapa transfoma kwa hiyo kama wewe ni mchimbaji na
unataka uchimbaji wao uwe wa kisasa,utajaza fomu itakayowezesha kuendesha
mashine zenu za kuchakata madini”Alisema Dkt Kalemani
Hata hivyo aliwasihi wachimbaji wadogo kutumia fursa ya umeme ili kuleta tija katika uchumbaji wao na hivyo kuweza kuongeza pia ufanisi mkubwa na alimtaka Mkandarasi na Tanesco kufikisha umeme katika Kijiji hicho ndani ya siku 20.

No comments