Breaking News

BIASHARA UNITED 2-0 NDANDA SC (TPL - 11/03/2019)



Dakika nane za kipindi cha pili zimetosha kuipa Biashara United ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma. Mabao ya wenyeji Biashara United yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 51 na George Makang’a dakika ya 58. Ushindi huu umeiongezea pointi tatu muhimu Biashara United, na kufikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kusalia katika nafasi ya 19 juu ya African Lyon yenye pointi 22 na Ndanda SC yenye pointi 33 katika nafasi ya 17.


Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.

BOFYA HAPA

No comments