Breaking News

MIRIAM ODEMBA NDANI YA TANZANITE WOMEN FORUM & LUNCH



Mwanamitindo wa Kimataifa, Miriam Odemba akiwa katika Mavazi ya Wabunifu wa mitindo mbalimbali wa Tanzania akiwemo Khadija Mwanamboka, Irada style na Katty Collection




Kuna msemo unasema “Asiyemshukuru Binadamu mwenzie kamwe hawezi kumshukuru Mwenye Mungu”. JUKWAA LA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MKOA WA DAR ES SALAAM (JUWADA), kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi maarufu BI.KHADIJA MWANAMBOKA kwa pamoja tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioshirikiana nasi kwa hali na mali kuhakikisha tunafanikisha tafrija yetu ya “Tanzanite Women Forum & Lunch 2019”.


Kwa hakika kungekuwa na maneno zaidi ya kusema ‘Asanteni Sana’ basi tungeyatumia hayo kuonyesha ni jinsi gani tunathamini na kutambua msaada wenu katika kufanikisha shughuli yetu ambayo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kufungua sehemu ya kuwapatia ujuzi tofauti wanawake wa Jukwaa. Kwa kupitia programme ya Bi Khadija Mwanamboka “Ujuzi Initiative”wanawake hawa watapatiwa Ujuzi mbalimbali wa mikono. Kipekee kabisa JUWADA tunamshukuru sana Bi Khadija Mwanamboka kwa kukubali kushirikiana nasi na zaidi kazi kubwa aliyoifanya kufanikisha “Tanzanite Women Forum & Lunch 2019”.


Kwa umuhimu wa pekee tunaomba kutoa shukrani zetu kwa kila mmoja wenu . Tunaomba kuanza kwa kuwashukuru wadhamini wetu wakuu walioweza kufanikisha shughuli yetu ambao ni ANUFLO INDUSTRIES LTD kupitia product ya “HEDHI MENSTRUAL CUP”. Tunawashukuru sana SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha eneo la kusomea wanawake hao.


Lakini pia tunaomba kuwashukuru wadhamini wengine wote ambao waliweza kwa namna moja ama nyingine kufanikisha shughuli yetu WAKIWEMO I4ID INCLUSIVE DEVELOPMENT, DARLING HAIR TANZANIA, COOL BLUE PURE DRINKING WATER. Tunaomba kuwashukuru kipekee wanawake waliojitolea thamani zao kwa ajili ya kufanya mnada akiwemo LEY JEWELLERS asante sana kwa seti ya Tanzanite. JACQUELINE MASSAWE JEWELLERS tunakushukuru sana kwa kututengenezea “Uhuru Wings” ambayo ni mkufu wa kipekee, NYUMBANI DADAZ NA ROSE VALENTINE asante sana kwa Maasai jewellery nzuri. Grano Foods Ltd na Rona products tunawashukuru mno kwa kutoa zawadi kwa wanawake.


Kipekee tuwashukuru wabunifu wa mavazi ambao mlifanya kazi kubwa sana kufanikisha show yetu akiwemo IRADA STYLE, MALIKA DESIGNER, ASYA KHAMSIN, KATTY COLLECTION, MUSTAFA HASSANALI, MGESE CICI DESIGNS NA ZAMDA GEORGE asanteni sana. Marafiki zetu na wadau wa maendeleo mliojitolea muda wenu mwingi kuhakikisha shughuli yetu inafana akiwemo Shamim Mwasha wa 8020Fashions na Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda. Wanamuziki chipukizi Abby Sollo na Mwalimu Habiba Lyengite. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya Shukrani. WASAFITV, Tanzanite Women Forum ya mwaka huu ndio ilikuwa ya kwanza kufanyika nanyi mkatupa heshma kubwa isyo kifani ya kuturusha LIVE kwa muda wote wa shughuli, ASANTENI SANA. MIRIAM ODEMBA kwako hatuna la kusema zaidi ya shukrani nyingi mno. Umekuja kutoka Paris kwa ajili ya “Tanzanite Women Forum & Lunch 2019”, na haukutaka chochote kutoka kwetu. Ubarikiwe kwa moyo wako wa kujitolea kwa ajili ya wanawake wenzio. Mwenyezi Mungu akuzidishie kila lenye kheri nawe. Kwa Wanawake wa Dar Es Salaam hususan wale wote mlioweza kujitokeza na kuja kutuunga mkono. Tunaomba mtambue shughuli isingefana bila ya uwepo wenu, hivyo tunawathamini na Kuwapenda sana. Asanteni sana kwa kuja. Tunatambua kwamba katika shughuli hakuwezi kila kitu kwenda sawa, hivyo kama kwa aina yeyote ile tuliwakwaza basi tunaomba Samahani kwani sisi ni binadamu na hakuna aliekamilika kati yetu.


Miriam Odemba akiwa katika mkufu wa kipekee "UHURU WINGS" uliotengenezwa na mbunifu wa madini Jacqueline Masssawe Jewelrs




























Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.

BOFYA HAPA

No comments