Breaking News

Julio apigwa chini Dodoma Fc


Uongozi wa timu ya Dodoma FC umevunja benchi lake la ufundi linaloongozwa na Kocha wake Jamhuri Kihwelo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo kwenye Ligi Daraja Kwanza na kumteua Joel Kakolanya kuwa kocha wa muda, akisaidiwa na Dotto Ligamna.

Julio aliiongoza na kukaribia kupanda ligi kuu msimu uliopita lakini akashindwa kwenye hatua ya mwisho kabisa na timu za Biashara United na Alliance zikapanda kwenye kundi hilo.

Msimu huu hali imekuwa mbaya zaidi kiasi cha kutishia timu hiyo kushuka daraja kutoka la kwanza mpaka la pili

No comments