Breaking News

Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea leo Huku Mechi Moja Ikisogezwa Mbele.


Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo katika dimba la Azam Complex na kuzikutanisha timu za Azam dhidi ya JKT Tanzania.

Wakati huohuo mechi ya  kati ya African Lyon na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe leo, imesogezwa mbele kwa siku moja, na sasa itapigwa kesho Jumamosini kutokana na Uwanja wa uhuru ambao ndio ungetumika kwa mcheo huo kutumiwa na watu wa michezo wa majeshi kwa siku nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema taarifa hiyo wameipokea juzi na hivyo kulazimika kuisogeza mbele hiyo mechi.

No comments