Makamba amwagiwa sifa baada kutoa tanzia yenye maneno ya hekima kwa Marehemu, Ruge Mutahaba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, January Makamba amemwagiwa sifa baada kutoa tanzia yenye maneno ya hekima aliyomuelezea Marehemu, Ruge Mutahaba jana KarimJee Jijini Dar Es Salaam.
Watu mashuhuri na wasio mashuhuri wamempa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter na yeye amewajibu kwa kushukuru; Kama inavyoonekana hapo chini.
"Nimesikiliza tanzia ya kaka @JMakamba kwa rafiki yetu Ruge nikiwa garini nakwenda Gerezani la Segerea. Ni tanzia yenye maneno ya hekima na yaliyomweleza Hayati Ruge kwa namna anayostahili. January amefanya kazi ya ‘Comforter In Chief’, amelihutubia Taifa. The best eulogy so far," ameandika Zitto.

No comments