Breaking News

Rais Magufuli akabidhiwa ramani ya Uwanja wa mpria utakaojengwa Jijini Dodoma



RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Morrocco nchini Tanzania Abdelillah Benry pamoja na waataalam wa ujenzi wa uwanja unaotarajiwa kujengwa Dodoma wenye ukubwa wa kubeba watazamaji elfu 85000.

Katika mazungumzo hayo Rais Magufuli aliweza kuoneshwa ramani ya uwanja huo ambao unaonekana wa kisasa ambao utakuwa ukitumika kwa michezo mbali mbali ikiweno mpira wa miguu, riadha na michezo mingine.

Baada ya mazungumzo hayo balozi wa Morrocco nchini Tanzania amesema kuwa kwa sasa Tanzania na Morrocco wapo katika mazungumzo ya utekelezaji wa miradi mikubwa miwili ambao ni kujenga msikiti na uwanja wa mpira.

“tumekuwa na mazungumzo kuhusiana na mipango ya maendeleo kati ya Morocco na Tanzania. Kwa sasa tuna miradi mikubwa miwili tunaisimamia, ambayo ni ujenzi wa msikiti pamoja na uzinduaji wa ujenzi wa Uwanja wa Soka”, alisema balozi Benry.

Uwanja huo ambao umetengewa hekari 143 unatarajiwa kujengwa eneo la Nara jijini Dodoma ambapo utaghalimu shilingi 56 bilioni sambamba na kituo cha michezo kitakachokuwa kilomita chache kutoka uwanja huo


Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.  BOFYA HAPA

No comments