Breaking News

Tetesi za soka barani Ulaya

 
Claudio Ranieri ambaye ni Meneja wa zamani wa timu za Chelsea, Leicester City na Fulham zinazo shiriki ligi kuu ya Uingereza, anakamirisha taratibu za kuichukua klabu yake ya zamani ya Roma baada ya upande wa ligi hiyo ya daraja la A kumfuta kazi Eusebio di Francesco.

Naye meneja wa zamani wa Manchester United, na Real Madrid, Jose Mourinho yuko tayari kurejea Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu ikumbukwe kuwa Mourinho alitimuliwa na Man U kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Zinedine Zidane, mwenye umri wa miaka 46, na meneja wa zamani wa Real Madrid, amehusishwa kujiunga na Chelsea pia anasakwa na klabu ya Uhispania na pia Juventus. Ikimbukwe kuwa ndiye kocha pekee aliyeweza kuutwaa ubingwa wa Ulaya 'UEFA' mara tatu mfululizo.

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, mwenye umri wa miaka 51, amefichua kuwa mazungumzo kuhusu hatma yake ya siku zijazo yamesitishwa hadi mwishoni mwa msimu, Hadi sasa Juventus ndio kinara katika msimamo wa ligi ya italia 'SERIA A' ikiwa na alama 72 na ikiwa timu pekee ambayao haijapoteza mchezo katika ligi hiyo.

Mshambuliaji wa Real Madrid Muhispania Isco, akiwa na umri wa miaka 26, ''amemkasirikia'' meneja wake Santiago Solari na ameelezea nia yake ya kuwasiliana na Manchester City ambayo ndio kinara wa ligi kuu Uingereza ikiwa imejikusanyia alama 71.

No comments