Wanafunzi 24 wajeruhiwa na radi huku mmoja akifariki dunia.
Wanafunzi ishirini na nne wa shule ya sekondari Mikindani iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wamejeruhiwa na radi huku mmoja akipoteza maisha katika tukio hilo liliowakuta wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao ya jana majira ya saa tatu asubuhi.
Tukio hilo limetokea majira ya saa tatu asubuhi ambalo limewakumba wanafunzi wa kidato cha tatu A wakati wakiendelea na masomo yao ambapo wanafunzi waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali.
Mkuu wa wilaya Mtwara, Evod Mmanda amesema kuwa jumla ya wanafunzi 24 wamejeruhiwa na mmoja aliyetambulika kwa jina la Abdul Masamba amefariki dunia katika tukio hilo huku Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula Dr. Lobikieki Kissambu amesema majeruhi wote waliopelekwa hospitalini hapo wanaendelea vizuri.
No comments