Breaking News

Ajira Ofisi ya Rais, TAMISEMI Waombaji Wapewa ushauri.



Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI, inaendelea kupokea maombi ya ajira za walimu zilizotangazwa hivi karibuni huku ikiwataka waombaji wote kuzingatia muda wa mwisho wa kutuma maombi hayo ambao ni tarehe 15 Machi, 2019.


Akizungumza Ofisini kwake kuhusu mwenendo wa waombaji hadi sasa Mkurugenzi wa TEHAMA, OR-TAMISEMI, Bw. Erick Kitali, alisema kwakuwa waombaji wanaomba kupitia mtandao wa (http://ajira.tamisemi.go.tz) ni vema pia wakazingatia tarehe ya mwisho ya maombi.


Kitali pia amewataka waombaji wote kuzingatia ukubwa wa nyaraka za viambatanisho huku akiwataka kuhakikisha zisizidi 1Mb au kuwa ndogo kadri iwezekanavyo, kutokana na walio wengi kupiga simu kwenye dawati la msaada na kutaka kujua ukubwa wa file kwa ajili ya ku-upload na kusema Nyaraka zote zinapaswa ziwe katika “format” ya “pdf” na sio format nyingine.


“Tunawashauri waombaji wote wa nafasi hizi za kazi zilizotangazwa kuzingatia maelekezo ambayo tayari tumeshayatolea muongozo kwa njia ya video (Video manual) na kuiwekwa kwenye Youtube ya Ofisi ya Rais TAMISEMI na kusambazwaa katika njia mbali mbali za mawasiliano, kwa urahisi wakujikumbusha na kufanya maombi ya kazi. Video hiyo ni fupi ya dakika. 10 tu” alisema Kitali.


Mbali na kutumia muongozo huo kwa njia ya video, amewashauri kutumia Progress bar wakati wa kuweka viambatanisho ili kujua kama unakaribia kumaliza ku-upload nyaraka husika na kutoikatisha njiani, “Ni Muhimu kutumia Progress bar wakati wa uploading” Alisisitiza Kitali.


Aidha, mfumo unatoa fursa ya mwombaji kuangalia hali ya maombi yake na kumwonesha kama amekamilisha mahitaji yote yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na nyaraka zote husika. Kila mwombaji anayo Profile yake, kwa msingi huo kila hatua lazima izingatiwe.


Mwisho Kitali amewataka waombaji hao kuendelea kuwasiliana na dawati la msaada kwa kutumia namba za simu ambazo zimetolewa na kusambaza kwenye tangazo la kazi lakini pia kwenye muongozo wa video. Vile vile, mtandao ambao waombaji wapo ni muhimu kuwa unafanya kazi vyema.


“Sisi tunasema TAMISEMI YA WANANCHI, hivyo tunajukumu la kuwahudumia wananchi wote kwa juhudi na maarifa yote” alihitimisha Mkurugezi huyo.


Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa OR-TAMISEMI, imendelea na uboreshaji wa Mifumo mbali mbali ya sekta ya umma katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ambapo hatua ya watu kuomba kazi kupitia matandao ni mafanikio makubwa katika ulimwengu wasasa.


Anaandika Atley Kuni- OR-TAMISEMI

No comments