Breaking News

Zifahamu rekodi alizoweka Ronaldo katika michuano ya UEFA, Aongea kwa hisia baada ya mchezo wao dhidi ya Atletico ‘Juventus walijua thamani yangu ndio maana wakanisajili’.



Cristiano Ronaldo alisajiliwa ili kuipatia Juventus ushindi wa ligi ya mabingwa – na huenda akafanikisha ndoto hiyo. Nyota huyo raia wa Ureno alionesha umahiri wake katika soka ya barani ulaya baada ya kuiwezesha klabu hiyo ya Italia kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuinyuka Atletico Madrid.

Kulikuwa na hofu huenda Juve huenda ikaondolea katika hatua ya muondowano baabda ya kufungwa mabao mawili katika awamu ya kwanza ya michono hiyo.

Ronaldo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 27 baada ya kuruka juu zaidi ya mlizi wa Atletico Juanfran na kuipatia Juvematumaini ya kubadilisha mkondo wa mchezo wao wa awali ambapo walifungwa 2-0


Dakika nne baada ya muda wa mapumziko, alifunga bao la pili – dhidi ya timu ambayo haijawahi kufungwa katika mechi tano zilizopita.

Wakati Federico Bernardeschi alipolemewa kupenya lango la Atletico na Angel Correa, ni mtu mmoja tu alingeliweza kufanya miujiza ya katka dakika nne za mwisho za kuamua nani atakaye fuzu kwa robo fainali

Hya ni baadhi ya rekodi ambazo Ronaldo amefanikiwa kuziweka katika Michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya UEFA.
Ronaldo amefunga jumla ya mabao 125 katika mashindano ya vilabu bora vya soka barani ulaya – Ushindi huu umefungua pengo la mabao 18 dhidi ya Lionel Messi katika orodha ya wafungaji bora wa mabao.
Ronaldo amefunga hat-tricks nane katika Champions League akiwa sawa na Messi.
Ronaldo anasalia katika nafasi ya kuongeza ushindi wake wa mara tano wa taji la Champions League- Ni nyota wa zamani wa Real Madrid Francisco Gento, ambaye ameshinda vikombe vingi Ulaya.
Ina karibu miaka minne tangu timu inayomjumuisha Ronaldo imekaribia kuondolewa katika Champions League lakini akabadilisha mkondo wa mchezo na kushinda kwa mara ya nne mtawalio.
Ronaldo ndio mchezaji pekee aliyofunga hat trick mara tatu akiifunga Atletico Madrid,2012,2016,2017 na 2019 katika michuano yote.
Mchezaji mwenye magoli mengi ya UEFA aliyofunga akiwa na zaidi ya miaka 30.goli 51,Zlatan 24,Drogba 23 na Inzaghi 19.
Mchezaji pekee aliyefanikiwa kuzisaidia timu zake kushinda katika michezo ya fainali akishinda fainali 5.
Mchezaji pekee aliyefanikiwa kufunga magoli katika michezo 6 ya UEFA wakiwa kwenye makundi.
Mchezaji pekee aliyefanikiwa kushinda tuzo nyingi za mchezaji bora wa UEFA akishinda mara 4.


‘Hii ndio sababu wamenileta hapa’

Ronaldo alijiunga na Juventus kutoka Real Madrid msimu uliyopita kwa kima cha euro milioni 99.2 na kuandikisha rekodi ya uwa mchezaji wa soka anayelipwa feha nyingi zaidi.

Jukumu lake kubwa lilikuwa kuisaidia kablu hiyo ya Turin kushinda ligi ya mabingwa.

“Hii ndio sababu Juventus ilinileta hapa, ili kusaidia kufanya vitu ambavyo havijawahi kufanywa,” alisema Ronaldo, ambaye sasa amefunga mabao 18 katika mechi 14 za hatua ya muondoano katika ligi ya mabingwa.

“Ilikuwa usiku maalum kwa timu yetu bila na bila shaka imekuwa hivyo .

“Ari hii inahitajika ili kushinda Champions League. Tulifurahia mchezo wetu. Atletico ilikuwa timu kali lakini sisi pia tulikuwa imara. Tunasubiri kuona kile kitakachofanyika.”

Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.BOFYA HAPA

No comments