Serikali yapokea msaada wa vifaa kinga kutoka China
Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa vifaa kinga vyenye thamani ya Yuan 2,150,00 sawa na shilingi 700,759,268 kutoka Serikali ya China.
Msaada huo umetoleowa leo katika Bohari ya Dawa (MSD) na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mabula Mchembe.
Prof. Mchembe amesema kwamba msaada huo umekuja wakati mzuri kwani utawasaidia watumishi wa afya katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19).
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mabula Mchembe na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe .Bi. Wang Ke wakitia saini nyaraka za makabidhiano ya msaada wa vifaa kinga vyenye thamani ya Yuan 2,150,00 sawa na shilingi 700,759,268 kutoka Serikali ya China.
No comments