Tatizo la kusikia kuongezeka maradufu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kwamba mpaka kufikia 2050 tatizo la usikivu litaongezeka maradufu kwa wananchi.
Waziri Ummy amesema hayo leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya usikivu duniani, ambapo ametoa rai ya watu kuepuka kelele ili kuzuia tatizo hilo.
Amesema kwamba mpaka sasa zaidi ya asilimia 5 ya watu duniani wana tatizo la usikivu.
"Tatizo hili litaongezeka maradufu ifikapo 2050. Kila mmoja wetu achukue hatua kujikinga nalo. Epuka kelele na pia kusikiliza mziki kwa kutumia spika za masikioni", amesema Waziri Ummy.
No comments