Breaking News

JICHO LANGU:UJINGA WETU NDIO MALIPO YA SOKA LETU,UJINGA WETU NDIO FAHARI YETU



“Mgogoro” Ni kutofautiana, baina ya watu, kupingana, kutoafikiana katika jambo fulani au mawazo fulani.

Hayo yote hutokea kutokana na uhitaji wa masilahi kwa manufaa ya mtu ama watu mmoja kutaka ukweli huku mmoja kutaka ubinafsi.

Tumekuwa wepesi kusahau ya nyuma na kutazama hapa tulipo na kuangalia kule tuendako licha ya kuwa wataalam wa Kiswahili husema kila uchao ya kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha hili ni neno lenye maana kubwa ikiwa tutalielewa.

Tuache hayo niangazie ujinga na fahari yetu ya Soka,imekuwa ni desturi kwenye Soka la nchi hii kuibuka migongano kutokana na baadhi kuwa na masilahi fulani huku wengine wakisalia kupiga miayo huu umekuwa ugonjwa wa kuibuka kwa migogoro ndani ya timu zetu.

Imekuwa fahari kwetu kuyasahau yaliyotukumba awali na kuibua majanga mapya pasipo kutambua madhara yake baadae,elimu tumepewa kipi kigumu kuitumia?.Mwaka 2011 Yanga sc iliingia kwenye sakata la kutaka uongozi wa Nchunga uondoke wakati timu inapambana kutafuta ubingwa wa ligi majibu ya mgogoro huo kama si madhara/athari yaliletwa na kutandikwa na Simba sc goli tano.

Ni fahari ipi ya ujinga inalengwa katika soka hili la timu zetu,tuliwashuhudia Simba sc tangu waingie katika zengwe la kutopenda uongozi wa Ismail Aden Rage figisu zikafanikiwa mwisho Rage akaacha timu lakini ujinga walisahau kuifanya timu iwe ina shinda kuunda mgogoro katika wakati mgumu ni lazima utegemee ugumu uliotaka ndicho kiliwapata mateso hayo walipata hadi wanakuja kuingia katika mfumo bora hivi karibuni.

Hivi karibuni limeibuka jipa kwa klabu ya Yanga sc baada ya viongozi wake kujiuzulu ila kwakuwa hatuoni mbele wala kukumbuka ya 2011 wameamua kujenga mgogoro wa kuona fulani alikuwa anafaa hivi wanashindwa kuangalia kipi kifanyike ili timu ipate ubingwa?.

Unajenga akili kumtazama anaetoka mwenyewe unaacha kuangalia mbadala wake na mweye sifa ya weledi wake huku timu ina kibarua kigumu cha kutafuta taji ambalo walipoteza unategemea nini?.Elimu zetu ni za kukuza tatizo badala ya kupunguza matatizo tutafika?.Fahari hii wategemee jibu.

Mtazamo wangu kwenu wapenzi wa kandanda migogoro imeletwa ili iwe changamoto ila si kuikuza zaidi ili ufanikiwe lazima utumie mwanya wa tatizo la awali ila ukifanya tatizo sehemu ya sifa kwa kulikuza ukubali kukosa mazuri ya mbele hivyo mnapaswa kukumbuka athari za migogoro hii ili kuweza kujiimarisha mapema.

Kama elimu zenu zingefaa zisitumike  kumjadili Dr Jonas,usikae kumjadili Manji ama badala yake angalieni mfanyeje timu itoke kwenye majanga msiwe watu wa sifa yaani kutaka kuongea katika vyombo vya habari tu.

Ikiwa migogoro itatawala malipo yake timu itaboronga na ubingwa kukosa fahari hii itawarudisha zama za 1994,1993 kuandaa timu mpya lakini bado itavurunda.

Beki Wa Kati 0653652483

©Sports Star Tz 

No comments