Breaking News

KIKOKOTO CHA AUSSEMS, HESABU ZAKE ZILIFELISHWA NA WACHEZAJI.



Ukitazama possession simba waliongoza kwenye First half na hata Second half walipokuwa wamefungwa goli tano, sasa unajiuliza Simba ilizidiwa nini?

Simba ilizidiwa sio uwezo wa kuuchezea mpira, Ilizidiwa Experience tu, experience  ya kucheza mechi kubwa, experience ya kutumia makosa, muda wa kujilinda na muda wakushambulia na kuheshimu mpinzani......kikubwa zaidi wachezaji wa Simba walizidiwa uwezo wa kimaamuzi na mchezaji mmoja mmoja wa As Vital....Simba wanahitaji kufuzu mara mbili tena ili wawe compitent na ubora waliokuwa nao Vital.

Kwa hapa walipofikia angalau wamepata funzo la kujua kucheza mechi kubwa za nje ya nyumbani na jinsi ya  kuwa na ukomavu wa kutimiza majukumu. Walinzi wasimba walikuwa wanajisahau kuwa washambuliaji wa AS Vital ni wa daraja la juu na walicheza fainali mwaka jana, wakati kona zikipigwa washambulizi wa Vital walienda kumziba Manura, ili asione muelekeo wa mipira walinzi wasimba walibweteka tu na hata hawakufuta move za mipira iliwakawanie mipira hewani walisimama tu.

Eneo la kiungo la Simba linapaswa kuwa na machaguo mawili liweze kushambuli kwa kutengeneza nafasi, lakini pia liweze kupokonya mipira na kuificha pindi linapozidiwa, jana hilo halikuonekana, ndio maana kagere na Okwi walipotelea kwenye kiungo cha As Vital.

Bado kuna nafasi kwa timu zote ila sasa Aussems anapaswa kushinda mechi zote nyumbani na kutafuta sare moja pale algeria.

Na @hebron_m_adimin

No comments