WHATSAPP WAJA NA SHARTI LA KUDHIBITI 'FAKE NEWS'
WhatsApp imetangaza masharti ya kiwango cha utumaji ujumbe kwa watumiaji wake kwenda kwa mwingine (forwarding sms) ambapo kwa sasa mtumiaji atakuwa na nafasi tano tu za kutuma ujumbe huo kwa mara moja lengo likiwa ni kuongeza jitihada za kukabiliana na usambazaji wa taarifa za uzushi /uongo (fake news).
Mmiliki wa biashara ya mtandao wa Facebook yeye tayari alishatambulisha sera hiyo nchini India miezi sita iliyopita.
Hatua hiyo imefuatia kuwepo kwa idadai kubwa ya makundi ya watu wanaodaiwa kujiua kutokana na taarifa hizo za uongo zinazosambazwa kupitia huduma hiyo ya WhatsApp.
Mpaka sasa, watumiaji wa mtandao huo walikuwa na uwezo sehemu yoyote duniani kutuma ujumbe kwenda kwa watumiaji wengine hadi 20 kwa wakati mmoja.
Mabadiliko hayo ya sheria hizo yametangazwa leo huko Jakarta, Indonesia katika hafla maalum huku nchi hiyo ikitarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi Aprili mwaka huu.
No comments