Breaking News

Waziri Ummi Mwalumu Afanya Ukaguzi wa Ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefanya kazi ya kukagua ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga!. .

Katika ukaguzi huo Waziri Ummy amesema Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) limekamilika Ndani ya wiki 2, na kuahidi Wizara italeta shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto.

Pia amesema kuwa anataraji kuleta fedha kwa ajili ya Jengo la Huduma za Uchunguzi na Upasuaji katika wiki chache zijazo.

"Kazi ya kukagua ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga!. Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) limekamilika. Ndani ya wiki 2, Wizara italeta shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto. Pia tunataraji kuleta fedha kwa ajili ya Jengo la Huduma za Uchunguzi na Upasuaji ktk wiki chache zijazo. Lengo  letu ni kukamilisha ujenzi wa majengo ya Awamu ya Kwanza ili tuanze kutoa huduma kwa Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kabla ya mwisho wa mwaka huu 2019."



Aidha Waziri Ummy ametembelea Kituo cha Afya Kambarage, kilichopo Manispaa ya Shinyanga na kujionea Ujenzi wa majengo muhimu kwa ajili ya huduma za uzazi wa dharura ikiwemo upasuaji wa kutoa mtoto tumboni (CEMONC) unaendelea vizuri. Kwa mujibu wa taarifa aliyoichapusha kwenye ukurasa wake wa instagram ameandika:

"Mkurugenzi amenihakikishia kazi itamalizika by 15 Feb. 2019. Hali ya utoaji huduma inaridhisha, dawa muhimu zinapatikana kwa zaidi ya asilimia 90."

"Hata hivyo nimeshuhudia msongamano mkubwa wa wagonjwa.  Tuna amini tutalimaliza tatizo hili mara tu tukikamilisha ujenzi wa majengo mapya ya CEMONC ya Kituo hiki na pia tukikamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambapo tutakabidhi kwa Manispaa ya Shinyanga Majengo ya sasa ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kuanzisha Hospitali ya Manispaa." 

No comments