Breaking News

Baada ya kumtimua timu yamrejesha kocha wake


Klabu ya soka ya Singida United, imemrejesha kikosini kocha aliyeipandisha timu hiyo kwenye ligi kuu msimu wa 2017/18, Fred Felix Minziro baada ya kuwa nje ya kikosi kwa takribani miaka miwili.


Taarifa ya Singida United leo, imeeleza kuwa wamefikia uamzi wa kufanya kazi na kocha huyo tena ili kuimarisha makali ya kikosi chao katika michuano mbalimbali wanayoshiriki.

''Katika kuimarisha benchi la ufundi, Minziro ameungana na benchi kumsaidia kocha mkuu Dragan Popadic, tayari ameshasafiri na kikosi ambacho kipo mkoani Mbeya kwaajili ya mchezo dhidi ya Mbeya City'', imeeleza.

Singida hawajaisahau kazi nzuri aliyoifanya Minziro katika ligi daraja la kwanza msimu wa 2016/17 ambapo aliipandisha timu ligi kuu na kisha kupoteza kazi kwa kocha Hans van der Pluijm aliyeifundisha timu hiyo msimu wa 2017/18 na kuisadia kumaliza katika nafasi ya 4 pamoja na kucheza fainali ya kombe la shirikisho ASFC. Singida imekuwa haina mwendelezo mzuri wa matokeo msimu huu kiasi cha kubadilisha makocha kutoka kwa Hemed Morocco aliyeanza msimu kwenda kwa Dragan Popadic ambaye ndiye anaendelea na timu kwasasa.

No comments