Bandari Mpya yajengwa Muleba
Hayo yamesemwa na mbunge wa Muleba Kusini Profesa, Anna Tibaijuka ambapo amesema kuwa halmashauri inatumia bandari hiyo iliyojengwa Mwalo wa Katunguru kuongeza mapato ya ndani kila mwaka
”Bandari hiyo na iliyojengwa na halmashauri ya wilaya katika Mwalo wa Katunguru, zinaongeza mapato yanayoboresha huduma za kijamii pia kuimarisha doria zinazodhibiti uvuvi haramu” Amesema Tibaijuka
Aidha, wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria majini wilayani humo wameiomba halmashauri ya wilaya hiyo kuwapunguzia ushuru wa tozo ya Shil. 3.6 milioni kwa mwaka ya kusafirisha abiria kwenda visiwani na kurudi ili wasipitie njia za panya
Kwa upande wake, Katibu wa kikundi cha wamiliki wa vyombo hivyo, Masudi Ibrahimu amesema tozo inayochukuliwa na halmashauri kila siku ni Sh. 10,000 kwa boti moja haiendani na mapato kwa wamiliki wa vyombo hivyo na wanaweza kufilisika.
Naye Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi, Richard Ruyango amezindua kikundi hicho katika Mwalo wa Magarini wilayani humo huku akiwataka wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria majini kufanya kazi kwa kulinda usalama wa wateja wao.
No comments