Breaking News

Kamati ya Bunge yataka uchunguzi mauaji ya watoto Njombe



 Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imependekeza Serikali kufanya uchunguzi wa haraka na kuwachukulia hatua kali wote watakaobainika kuhusika na mauaji ya watoto mkoani Njombe.


Hayo yameelezwa leo Alhamisi Februari 7, 2019 bungeni jijini Dodoma na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Juma Nkamia akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo.


“Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la ukatili wa kijinsia na watoto hususan katika mkoa wa Njombe ambako watoto wanaendelea kuuawa jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya nchi yetu na matakwa ya makubaliano ya kimataifa, lakini ni kinyume na haki za binadamu,” amesema Nkamia.

No comments