Mabaki ya ndege iliyombeba mchezaji wa Cardiff City Emiliano Salas yamepatikana
David Mearns wa taasisi ya "Society of Blue water recovery" aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter " Mabaki ya ndege yalipatikana siku ya Jumapili asubuhi".
Ndege hiyo ndogo inasemekana ilipotelea kaskazini mwa visiwa vya Guernsey mnamo siku ya Januari 21.
Sala 28 pamoja na rubani David Ibbotson walikuwa wakitokea Nantes kuelekea Cardiff ambako ndipo makao ya timu Cardiff City ambayo Sala alikuwa ametoka kusaini mkataba wa kuichezea wenye thamani ya Euro milioni 17.
Mchezaji huyo inasemekana alikwenda ufaransa kuwaaga wachezaji wenzake wa Nantes FC, timu ambayo alikuwa akiichezea.

No comments